Simba kuwavaa Mtibwa bila beki benchi

Thursday May 16 2019

 

By THOMAS NG’ITU

KIKOSI cha Simba dhidi ya Mtibwa kimetoka huku kukiwa na mshtuo baada ya kukosekana beki wa kati katika upande kikosi cha akiba cha mchezo huo.

Kikosi kinachoanza ni Aish Manula, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein, Yusuf Mlipili, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Clatous Chama, Haruna Niyonzima, John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi.

Wakati upande wa akiba yupo Deogratius Munish, Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, Mohammed Ibrahim, Adam Salamba na Rashid Juma.

Hivyo kama ikitokea beki ameumia katika mchezo huu kutakuwa na kibarua kigumu kwa Simba kwani nje hakuna mchezaji ambaye ni beki asili wa kati.

Kocha  wa Simba, Patrick Aussems hata katika mabadiliko yake uwanjani amekuwa akiangalia zaidi katika eneo la katikati kuliko sehemu nyingine yoyote.

Advertisement