Smalling amsimamisha Lionel Messi La Liga

Sunday April 14 2019

 

Kiungo wa Barcelona, Lionel Messi, amelazimika kupumzishwa mchezo wa jana dhidi ya Huesca, huku Luis Suarez akisimamishwa.

Miamba hiyo ya Catalans itakuwa na kazi dhidi ya Manchester United Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne ijayo ikiwa na hazina ya bao 1-0 iliyopata kwenye Uwanja wa Old Trafford Jumatano iliyopita.

Mchezaji mwingine ambaye alikosekana jana ni Sergio Busquets ambaye amepumzishwa pia kuisubiri Man United, Gerard Pique amefungiwa wakati Ivan Rakitic na Sergi Roberto wote ni majeruhi.

Hata hivyo, kikosi cha Ernesto Valverde, kabla ya mchezo wa jana, kilikuwa na pointi 11 kileleni mwa La Liga.

Kwa upande wake Messi, alimwambia Chris Smalling amemuumiza lakini anaamini kuwa Smalling hakudhamiria kufanya kilichotokea.

Beki huyo wa Manchester United alimuumiza Messi wakati wa mchezo wao walipokuwa wakiwania mpira kwenye Uwanja wa Old Trafford na Messi akaenda chini.

Baadaye Smalling alimvuta Messi lakini kabla alipitisha mikono wake usoni na kumgonga kwenye pua kiasi cha kumfanya avuje damu.

hata hivyo, Messi alipata huduma ya kwanzxa na kuendelea na mchezo, lakini aliiambia BBC Radio 5 kwamba beki huyo wa Manchester United alikwenda na kumpa mkono kumpa pole.

Advertisement