Tanzania yatupwa Kundi D saizi yake

Monday February 17 2020

 

Dar es Salaam. Tanzania imepangwa Kund D pamoja Zambia, Guinea na Namibia katika mashindano ya CHAN2020 Cameroon.

Kupangwa kundi hilo linaofanya Tanzania kukwepa vigogo wa mashindano hayo.

Tanzania inashiriki mashindano hayo kwa mara yapili inakutana na Zambia katika mechi ya ufunguzi ya kundi lake.

Katika droo ya upangwaji wa makundi ya mashindano hayo mwaka huu,iliyofanyika jijini Yaounde, Cameroon na kuongozwa na nyota wawili wa zamani wa nchi hiyo, Salomon Olembe na Stephen Tatah, wenyeji wamepangwa kundi A sambamba na Mali, Burkina Faso na Zimbabwe.

Mabingwa watetezi Morocco wao wameangukia katika kundi C wakiwa sambamba na Rwanda,, Uganda na Togo wakati kundi B litakuwa na timu za Libya, DR Congo, Congo na Niger.

Bingwa wa mashindano hayo atapatiwa kitita cha Dola 1.25 milioni (zaidi ya Shilingi 2.5 bilioni).

Advertisement

Tanzania inashiriki mashindano hayo kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo mwaka 2009

 

Kundi A – Cameroon, Mali, Burkina Faso, Zimbabwe

 

Kundi B- Libya, DR Congo, Congo, Niger

 

Kundi C – Morocco, Rwanda, Uganda, Togo

 

Kundi D – Tanzania, Namibia, Guinea, Zambia


Advertisement