Viingilio vya Simba, mashabiki washindwe wenyewe

Tuesday January 8 2019

 

By OLIPA ASSA

Simba imetangaza viingilio vya mechi yao na JS Saoura ya Algeria, hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa Afrika, utakaopigwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumamosi ya wiki hii.

Kwa mujibu taaarifa ya Simba iliyowekwa kwenye mtandao wao wa Instagram, ilionyesha viingilio hivyo ambapo kima cha juu kitakuwa 100,000 kwa platinums, wakati VIP B itakuwa shilingi 10,000.

Kwa viti vya mzunguko ambako ndiko wanakaa asilimia kubwa ya mashabiki itakuwa Shilingi 50,00 kwa mchezo huo unaotazamwa kuwa mgumu zaidi.

Kutokana na viingilio hivyo kocha wa zamani wa Njombe Mji, Mlage Kabange ametoa maoni kwamba kwa viti vya mzunguko wangefanya Shilingi 3,000 ili kupata watu wengi zaidi wa kuiunga mkono timu.

"Nguvu ya mashabiki ni kubwa hata kama wageni wapo moto kuna kiasi watapoa, pia waendelee kufanya hamasa ili watu waweze kufika kwa wingi siku hiyo," anasema.

Advertisement