Yanga kurejea Dar kesho, Zahera ajigamba

Tuesday September 10 2019

 

By Saddam Sadick, Mwananchi [email protected]

Mwanza. Kikosi cha Yanga kinatarajia kufanya mazoezi ya mwisho kesho Jumatano Septemba 11, 2019 kabla ya kurudi jijini Dar es Salaam kucheza na Zesco ya Zambia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera amesema baada ya kumaliza mechi zao za kirafiki, kesho watafanya mazoezi ya mwisho asubuhi katika uwanja wa Nyamagana na baada ya hapo watapanda ndege jioni kwenda Dar es Salaam.

Amesema kambi ya Mwanza imekuwa na faida, wanatarajia kufanya vyema katika mchezo wa kwanza utakaochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

"Kesho (Jumatano) tutafanya mazoezi ya mwisho hapa uwanjani asubuhi baada ya hapo jioni tutapanda ndege kwenda Dar es Salaam kujiweka tayari na mechi ya Jumamosi. Kwa ujumla kambi imekuwa nzuri na tunatarajia kupata mafanikio" amesema Zahera.

 

Advertisement