Davido: Mafanikio yangu ndio sababu ya kuchukiwa

Thursday August 1 2019

 

Nigeria. Mwanamuziki wa Nigeria,  Davido amedai wasanii wenzake wana chuki naye kwa kuwa amekuwa na mafanikio makubwa katika muziki.

Kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Davido ameweka video fupi na kuandika kuwa anapenda kuwashukuru mashabiki wanaomuunga mkono na kumpenda baada ya kuachia wimbo aliomshirikisha msanii wa Marekani, Chris Brown.

Davido ameeleza kuwa yupo tayari   kuzungumza kuhusu soko la muziki nchini Nigeria kwa kuwa analijua kwa zaidi ya miaka saba lakini hawajamuunga mkono kwa sababu ya chuki.

Kauli hiyo ya Davido imeonekana ni kama kijembe kwa wasanii wenzake  nchini Nigeria.

Wasanii wananichukia kwa sababu nilipewa fedha nyingi na baba kwa ajili ya kufanya muziki, kufanya vizuri na kutoa kazi nzuri.  Pamoja na kuwateka mashabiki  na hilo ndio  kosa langu la kuchukiwa,” amesema Davido.

Advertisement