Bambika 101 ya MCL Digital yamuingiza Msowoya nusu fainali Maranatha Awards

Dar es Salaam. Kipindi cha Bambika 101 cha MCL Digital kimemuingiza mwandishi wa gazeti la Mwananchi Tumaini Msowoya kwenye nusu fainali ya kinyang’anyiro cha tuzo za Maranatha Awards zitakazofanyika Mei 11 mwaka huu nchini Kenya.

Katika tuzo hizo Msowoya ambaye pia ni masanii wa muziki wa Injili, ameingia katika kipengele cha ‘Outstanding Kingdom Media Personality of Excellence’ akichuana na watangazaji wengine 15 huku Tanzania akiwepo yeye, Masanja Mkandamaji na Uncle Jimmy.

Tuzo hizo zinazoshirikisha mataifa mbalimbali duniani hufanyika kila mwaka na moja ya sifa ni lazma uwe muimbaji wa muziki wa Injili.

Akizungumza na Mwananchi kuhusu kufikia hatua hiyo, Tumaini alisema anamshukuru Mungu hii inaonesha namna gani vipindi vya MCL Dital vinavyotazamwak ikiwemo Bambika amcho huonyeshwa kila siku ya Jumapili kwenye youtube ya MCL Digital.

Kwa upande wa uimbaji alisema akiwa ndio kwanza ana miaka mitatu tangu angie kwenye muziki wa Injili watu wameweza kumtambua, jambo ambalo wengi wanaoimba muziki huo wangetamani iwe hivyo kwao.

Akieleza namna anavyoweza kupigiwa kura, Msowoya alisema, “unatakiwa kuandika Dr Tumaini Msowoya kisha acha nafasi, andika jina lako na eneo unaloishi unatuma kwenda namba +254710910515”.

Tumaini alianza kusikika kwenye muziki wa Injili mwaka juzi baada ya kuachia albamu yake ya kwanza ya auodio inayoitwa ‘Hakuna Matata’ iliyobeba nyimbo mbalimbali ikiwamo Ni Mwema, Amenitengeneza, Samehe na ‘Nina Furaha’ ambayo video yake aliiachia mwaka jana.