Diamond Platnumz, N’golo Kanté wang'ara tuzo za BOA Uingereza

Monday October 7 2019

 

By Evagrey Vitalis @MwananchiNews

Dar es saalam. Staa wa Muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz ametunukiwa tuzo ya “Philanthropic Endeavour Community Action” kutokana na mchango wake kwa Jamii kwenye tuzo za Best Of Africa “BOA” Jijini London, Uingereza usiku wa Jumapili ya Oktoba 6.

Tuzo za Best of Africa huwa zinawahusisha zaidi wanasoka pamoja na watu mashuhuri ambao wanafanya vizuri kutoka Africa, Diamond Platnumz ni mmoja ya mastaa waliohudhuria mwaka huu.

Star wa Bongo Fleva Diamond Platnumz kwenye usiku wa tuzo za BOA amekutana na beki wa zamani wa timu ya Taifa Uingereza na klabu ya Manchester United ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka Rio Ferdnand.

Ikiwa Mwaka huu zinafanyika kwa mara ya nane, Tuzo za BOA huwa zinawaleta pamoja watu mbalimbali ambao wanaunga mkono na kushiriki kwenye maendeleo na maadili ya kiuchumi katika bara zima, pamoja na kuwapa Tuzo washindi wa vipengele mbalimbali.

Baadhi ya watu wengine walioshinda usiku wa Jana ni pamoja na Fuse ODG, Wilfried Zaha, Mosamba, N’golo Kanté, Stormyz, Pia tuzo hizo zilihudhuriwa na watu wengine mashuhuri kama mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Uingereza na Klabu ya Manchester United, Rio Ferdnand.

Advertisement