Mfahamu mwanamke aliyechuniwa na Beyonce kisa Jay-Z

Saturday June 8 2019

 

By Evagrey Vitalis

Mambo ni mengi na muda ni mchache! Usiku wa jumatano june 5 ulipigwa mchezo wa fainali ya tatu ya NBA kati ya Golden state warriors na Toronto raptors, mchezo uliohudhuriwa na rapa Jay-z na Ubavu wake Beyonce katika uwanja wa Oracle Arena na kwenye tukio hilo bwana kuna mwanamke aliyechuniwa na Beyonce kisa Jay-Z.
Nicole Curan ni mwanamke aliyeonekana akiongea na Jay katika fainali ya tatu ya NBA ambapo ilionekana kama Beyonce hakupendezwa na kitendo kile na watu walibaki na maswali mengi sana hasa yule mwanamke ni nani.
Curan ni mke wa mmiliki ya timu ya Golden state warriors Joseph Steven Lacob, Mnamo 2006, Curran alikukutana na Lacob kwenye mashindano ya golf ya Pebble Beach hapo ndipo urafiki wao ulipoanzia hadi hivi sasa ni mume na mke.

Curan ni mke wa mfanyabiashara billionea anayemiliki timu ya Golden state warriors Lacob, mwenye umri wa miaka 63, anamiliki timu hiyo inayocheza mpira wa kikapu na ameingia ubia wa umiliki wa timu hiyo na Kleiner Perkins.
Baada ya Curan kuonekana kuongea na jay-z mashabiki wa beyonce waliamua kumfuata katika mtandao wake wa Instagram na kumshambulia kwa maneno makali na wengine kufikia hatua hadi ya kumtishia uhai wake na mashabiki walikurupuka bila kumjua Curan.
Curan aliibuka na kusema kwamba Jay alikua anahitaji kinywaji cha vodka soda na ikaleta kama mahojiano maana hakumtaka Jay kunywa kinywaji hicho.
Jay na Beyonce walihudhuria kutazama fainali ya tatu ya NBA ikiwa siku chache baada msanii Jay-Z  kutajwa msanii wa rap anayemiliki mpunga mrefu duniani, na katika fainali hiyo Golden walipoteza mchezo huo kwa alama 109 kati ya 118 za Raptors katika uwanja wao wa nyumbani.
Mashabiki wa Beyonce waliumbuliwa na ule msemo unaosema usijaji kitabu kabla hujakifungua ndani maana walimwandama curan bila kujua ni mke wa billionea wa timu iliyowafanya Jay na Beyonce kufika Oracle Arena kutazama timu hiyo ikicheza na Toronto Raptors.

Advertisement