Shilole atamani mwili wake wa zamani

Friday September 13 2019

 

By Asna Kaniki, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Muvi nchini Tanzania, Zuwena Mohammed maarufu Shilole hatimaye amefunguka kuhusu kunenepeana.

Shilole asiyekwisha vituko ikiwamo kupania kuzungumza lugha ya Kiingereza, ameapa kufanya mazoezi ili arudi kwenye mwili wake wa zamani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameweka picha yake ya zamani alipokuwa mwembamba na kuandika yupo kwenye mazoezi makubwa ya kurudi kwenye mwili huo.

“Nipo kwenye mazoezi makubwa saana kurudi huku tupeane moyo,” amesema

Katika picha yake ya pili iliyomuonyesha akiwa mwembamba zaidi na kuandika  “Daah yaani ni miaka miwili tu nyuma nasema na pambana na mazoezi.”

Licha ya usanii wake Shilole pia ni mjasiriamali wa chakula ambapo hivi sasa anamiliki eneo mwenyewe na kuhudumia watu mbalimbali wakiwemo watu maarufu.

Advertisement

Advertisement