VIDEO: Ulinzi wa Diamond wazua maswali hotelini

Wednesday September 25 2019

 

By Elizabeth Edward, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Ulinzi wa mwanamuziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz umeonekana kuwashangaza watu hasa wageni.

Leo Jumatano Septemba 25, 2019 Diamond ametinga katika hoteli ya Hyatt Regency iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam nchini humo akiwa na walinzi wake 11 waliovalia sare nyeusi na miwani ya rangi nyeusi.

Idadi kubwa ya walinzi hao ilionekana kuwashangaza watu waliokuwa wakiendelea na shughuli zao hotelini hapo huku baadhi yao wakiuliza kutaka kumfahamu Diamond.

“Who is this man?” alisikika akiuliza mwanaume mmoja mzungu ambaye alikuwa akimuuliza mmoja wa walinzi katika hoteli hiyo.

Mshangao ulionekana pia wakati anatoka ambapo walinzi hao walilizunguka gari lake kwa muda jambo lililowafanya watu waliokuwa nje ya hoteli kushangaa.

Msanii huyo alifika hotelini hapo kuhudhuria shughuli ya utambulisho wa Ubalozi wa Kampuni ya Bomet.

Advertisement

Katika mkataba alioingia wa ubalozi huo, Diamond atakuwa balozi wa sabuni ya unga ya Niceone inayozalishwa na kusambazwa na kampuni hiyo.

Advertisement