Breaking News

Utata Cheed na Killy kuondoka Kings Music ya Alikiba

Tuesday April 14 2020

 

By Rhobi Chacha

Zikiwa zimepita siku tano toka mwanamuziki wa bongo fleva Alikiba kutoa wimbo mpya wa Dodo, vijana wake wawili kutoka lebo yake ya  Kings Music,  Cheed na Killy wametangaza rasmi kuondoka kwenye label hiyo.
Wanamuziki hao kupitia akaunti zao za Instagram leo Jumanne, wameshukuru uongozi wa label hiyo kuwaongoza vyema kipindi chote walichokua wakiitumikia na wamesisitiza kuwa wamejitoa kwa kheri ili waweze kujiendeleza zaidi katika muziki wao na kwa namna yoyote ile wapo tayari kupokea ushauri na kushirikiana katika kazi zao na Alikiba.
Mmoja wa mameneja wa Alikiba,  Aidan Seif amesema, habari hiyo ya kujitoa kwa wanamuziki hao wameiona kwenye mtandaoni wa Instagram kama walivyoona watu wengine, na  baada ya hapo wamewapigia simu hawapatikani kwenye simu.
"Bada ya kuziona taarifa hizo, tumejaribu kuwapigia simu hawapatikani, hivyo hili suala hatukulifahamu kama wanajiondoa kwenye lebo ya Kings Music, tumeona kama watu walivyoona kupitia akaunti zao" amesema Seif
Ameongeza kusema kuwa, hakuna ubaya wao kujiondoa kwani pengine wamepata sehemu zaidi au ni maamuzi ya kutaka kujiendeleza wenyewe.
Kipindi cha nyuma AliKiba aliwahi kusema kuwa wasanii ambao wapo chini yake hawajawapa mkataba na yeye anachofanya ni kuwasaida na kama itafika muda watataka kuondoka wanaweza kuondoka na hivyo ndivyo ilivyotokea kwa wasanii wake hao wawili.
Kings Music chini ya Alikiba imeanzishwa mwaka 2017 baadhi ya nyimbo ambazo wamezitoa ni Toto, Mwambie Sina,  Rhumba na Masozy

Advertisement