Wema: Diamond ni rafiki yangu hatujagombana

Friday February 21 2020

 

By Nasra Abdallah, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu amesema msanii Diamond Platnumz ni rafiki yake na watu wasitafsiri tofauti wanapoona hajawahi kuwa na urafiki katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

Wema ameeleza hayo leo Ijumaa Februari 21, 2020 wakati akiingia makubaliano na kiwanda cha rasta cha rasta cha Angel kuwa balozi wa bidhaa zao.

Wema amesema suala la ‘kutomfollow’  Diamond katika mtandao huo ni makubaliano yao tangu walipokuwa na mahusiano.

Kuhusu uhusiano wake na mkali huyo wa Bongofleva, Wema amesema hawana ugomvi wowote, “kuna wakati hata tulitaka kuwa na kipindi katika  televisheni ya Wasafi. Kipindi ambacho tungefanya kwa kushirikiana mimi, Anti Ezekiel na Zamaradi Mketema, lakini yakatokea ya kutokea kikayeyuka.”

“Kama mnavyoona sasa, mimi nina App yangu ya Wema na Zamaradi  ana TV yake kila mtu anatengeza vipindi vyake huko.”

Advertisement