Barcelona yamtosa Paulinho

Monday July 9 2018

 

Barecelona Hispania. Klabu ya Barcelona ya Hispania, imewastusha wengi baada ya kumrudisha Guangzhou Evergrande kiungo wake wa kibrazil, Paulinho, iliyemsajili kiangazi cha mwaka jana.

Braca ilimsajili Paulinho, 29, kutoka Guangzhou ambako aling’ara sana akifunga mabao 22 katika mechi 84 alizocheza tangu aliposajiliwa mwaka 2015 akitokea Tottenham Hotspur ya England.

Hata hivyo kiungo huyo kutoka Brazil, aliyetua Barcelona 2017, alicheza mechi 34 za La Liga na kufunga mabao tisa.

Jambo la kushangaza ni kuwa Barca inamuuza kiungo huyo baada ya kung’ara katika fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia licha ya Brazil kutolewa na Ubelgiji katika ribo fainali.

“Klabu ya Guangzhou Evergrande inathibitisha kumpokea tena Paulinho atajkayecheza hapa kwa mkopo akitiokea Barcelona, alikocheza msimu mmoja”.