Uandishi wa kutafuta utatuzi wa changamoto

Uandishi wa kutafuta utatuzi wa changamoto

 

Mara nyingi kumekuwa na uan-dishi wa habari wa kukariri machungu, shida na matatizo ya mtu binafsi, kijiji na hata taifa. Huu ni uandishi wa kukumbushia shida na majanga. Ambacho mwandishi wa habari “mpi-tanjia” amekuwa akifanya, ni kutangaza shida na vilio na kuwaacha wahusika katika lindi la majuto bila fununu ya kinachoweza kufanyika kuondoa majuto.

Hana habari kwamba anaowaandika hawajui kuwa mahali fulani kulikuwa na shida, changamoto au matatizo ya aina hiyo lakini yaliishatatuliwa.Waandishi wa aina hii huitwa para-chute journalists au waandishi wa “mia-vuli.”

 Hawa hutua kwenye eneo la kuri-poti wakiwa na taarifa kidogo au bila taarifa yoyote kwa madai kwamba waki-fika huko wataona cha kufanya. Hawajui kwa undani tatizo au changamoto za eneo husika. Hawana uzoefu wa popote pale ambako waliishaona changamoto za aina hiyo zikishughulikiwa. Sasa wito mkuu katika uandishi wa habari unaolenga kuleta ufumbuzi, ni mwandishi wa habari kuwa katika eneo husika; kuelewa fika mazingira anamo-fanyia kazi; kujua furaha na karaha za jamii pale alipo; kufahamu historia ya watu na mazingira anayoripoti na kupanga kwa kadri mazingira yalivyo.

Mwandishi awe anajua jamii nyingine karibu au mbali na mahali anakofanyia kazi; changamoto au matatizo yanayo-sibu jamii hizo na iwapo kuliishakuwa na juhudi za kuyakabili; matokeo ya juhudi hizo na mazingira yake kwa jumla waka-ti anatafuta kuandika habari za mahali alipokwenda.Elimu ya darasani ni muhimu kwa maandalizi; lakini pia maarifa ya kuji-pekulia kwa njia ya kukutana na watu wa rika na viwango tofauti vya elimu na uelewa; na kuwa katika maeneo na nchi tofauti, ni muhimu pia.

Twende kwa mfano huu. Kijiji katika wilaya moja kinaweza kuwa kinashere-hekea ushindi ambao ni kuondokana na mapigano kati ya, na miongoni mwa, wakulima na wafugaji. Haya yalikuwa mapigano ya kugom-bea ardhi ya malisho na kilimo na yalii-shasababisha vifo vya watu 27; kuleta ulemavu kwa watu 61 na kufanya watoto kuacha kwenda shule kutokana na woga.Katika kijiji kingine katika wilaya ya mbali bado wana tatizo hilohilo. Lime-kuwepo kwa miaka saba. Sasa uandishi wa habari unaolenga suluhisho unata-ka mwandishi aliye katika kijiji chenye matatizo, atoke nje ya kijiji.

Aenda. Aone. Ahoji. Anukuu. Ahuishe na kufikiri jinsi ya kutoa andishi lenye lengo la kule-ta furaha.Kutoka nje ya kijiji kuna maana ya kusafiri, kusoma, kutafiti au kukutana na wenye maarifa na uzoefu – kuona vijiji vingine, ndani au nje ya nchi; kupa-ta uelewa, kuhemea maarifa na hati-maye kuandika kwa msingi wa kuondoa majonzi na kuleta faraja na furaha.

 Huku siyo kuiga; ingawa siyo viba-ya kuiga. Hapa kuna mazingira tofauti yenye matatizo yaleyale; na ambako suluhisho laweza kufanana au kuwa lilel-ile. Anayefukua, kulinganisha na kuweka bayana, anakuwa anatafuta suluhisho kwa maslahi mapana ya umma. Kuandika tatizo au juu ya tatizo na kukimbia, hakusaidii jamii unayoripoti. Kuonyesha tatizo lilivyo, kulilinganisha na jingine la aina hiyo mahali pengine; na kuonyesha lilivyotatuliwa, ndiko kun-aongeza thamani ya uandishi, andishi lenyewe na mwandishi.Kwahiyo, mwandishi wa habari za kuleta ufumbuzi anapaswa kuwa na uwezo wa kufanya uchunguzi wa jamii anayoandika juu yake na changamoto zake.Sharti awe na uwezo wa kuona, kufikiri na kuhoji. Weka msisitizo kwenye kuhoji: Kwanini hili liko hivi?

Kwanini liko hivi kwa muda wote huu? Liliwahi kutokea kwingine? Wapi? Lilitatuliwa vipi? Hii ndiyo maana mwandishi wa habari za kuleta suluhisho anapaswa kuwa na upeo mpana. Hakomei kwenye mapi-gano na vilio vya wakulima na wafu-gaji.

Anaweza kutafuta pia jinsi ya kuleta suluhisho kati ya wajasiriamali wachuu-zao bidhaa za mkononi na watawala wa majiji ya Dar es Salaam na Mwanza.Mwandishi anaona jinsi “mach-inga” (maduka yanayotembea) wana-vyofukuzwa kwa kutumia mgambo; kunyang’anywa bidhaa zao; kushitakiwa na kuswagwa nje ya jiji kila mgeni wa tai-fa anapokuja – kana kwamba ni uchafu.Wapi kwingine kulikuwa na changa-moto au tatizo kama hilo?

Walifanya nini? Hali ikoje sasa? Watawala na watawaliwa watajifunza kutokana na upeo wa mwandishi na wale aliokutana nao katika kutafuta suluhisho.Mifano mingine yaweza kuwa: wen-gine walifanikiwa vipi katika kilimo cha umwagiliaji; huduma kwa wajawazito; ujenzi wa Katiba inayozingatia uhuru wa mtu binafsi na jamii; siasa za nchi na utawala.Kwa kusoma, kupekua, kuhoji, kusafiri na kuona; mwandishi anajua kipi kili-fanyika wapi na jinsi kilivyofaniki-shwa.

Anapata pia njia mpya za ubu-nifu zinazoweza kutumika. Anaandika kwa shabaha ya kufungua mbongo za walengwa wake ili watende na kupata ufumbuzi.(Makala hii ilichapishwa mwaka 2018. Imerudiwa kwa kuongezewa mnofu kwa maombi ya wasomaji wetu sita; wanne wakijitaja kuwa wanafunzi)

Mhariri wa Jamii anapatikana: 0763670229