Mpango ataja sababu za kufungwa kwa biashara 7,000

Thursday June 08 2017
pic biashara

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango

Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango amesema, zaidi ya biashara 7,277 zilifungwa hapa nchini kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ushindani mkubwa wa kibiashara.

 Dk Mpango ameyasema hayo leo Alhamisi bungeni wakati akiwasilisha bajeti ya mwaka 2017/18.

Amezitaja sababu za kufungwa kwa biashara hizo kuwa ni usimamizi dhaifu, kuongezeka kwa gharama za kusimamia biashara na kutozingatia masharti ya biashara.

 

Advertisement