Afya ya Mbowe yaimarika, kuruhusiwa wakati wowote

Freeman Mbowe 

Muktasari:

Mbowe aliugua ghafla jana alfajiri na kuwahishwa hospitali ya Muhimbili

Dar es Salaam. Afya ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe imeimarika na  anaweza kuruhusiwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakati wowote kuanzia sasa.

Ofisa Uhusiano wa MNH, Neema Mwangomo ameiambia Mcl Digital leo Juni 19, kuwa kiongozi huyo anaendelea vizuri.

"Nimeongea na muuguzi anayemuangalia amesema afya yake iko vizuri na matibabu yake yamekwenda vizuri anaweza kuruhusiwa muda wowote,"amesema Mwangomo.

Hata hivyo, Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, amekataa kuzungumza na wanahabari.

"Nimeongea naye amenijulisha kuwa hayuko tayari kuzungumza na waandishi wa habari kwa sasa labda baadaye."