Weah arithi serikali iliyo mfilisi

Muktasari:

Masalale! Mwanasoka huyo mkongwe anashika usukani wa kuiongoza Liberia, moja ya nchi masikini duniani katika wakati ambao uchumi umeanguka.

 

Monrovia, Liberia. Rais mteule George Weah ambaye anatarajiwa kuapishwa Januari 22 atarithi changamoto kadhaa zinazokatisha tamaa ikiwemo ya kurekebisha uchumi uliozorota.

Changamoto nyingine zinazomkabili ni kutengeneza ajira na nafasi za kusoma katika nchi hiyo ambayo asilimia 85 ya vijana wasio na kazi.

Ushindi wa asilimia 61.5 aliopata Weah katika kinyang’anyiro cha urais umekuja na mtarajio makubwa kutoka kwa wananchi hasa vijana kwa hiyo kutimiza matarajio yao ni kazi nyingine kubwa.

Matarajio yaliyojengwa kwa miongo kadhaa yakiwa yamegubikwa na uhaba wa fursa kwa watu wa kipato cha kati na cha chini sasa yamechochea watu kutaka yaboreshwe maisha ya watu.

Masalale! Mwanasoka huyo mkongwe anashika usukani wa kuiongoza Liberia, moja ya nchi masikini duniani katika wakati ambao uchumi umeanguka.

Mara baada ya kutia saini Bajeti ya Taifa ya mwaka 2017/18, Rais Ellen Johnson Sirleaf aliitisha kikao maalumu na wabunge akiwataka wapiti upya bajeti kutokana na uwezo mdogo wa serikali kukusanya dola za Marekani 563.6 milioni zinaohitajika.