Fast Jet yashindwa kutua Songwe

Muktasari:

  • Ndege hiyo ilitarajiwa kutua leo saa 2.00 asubuhi, lakini  ilipofika anga la jiji la Mbeya ilikumbana na ukungu ulioambatana na mvua kubwa ikinyesha.

Mbeya. Ndege ya Kampuni ya Fast Jet imshindwa kutua kwenye Uwanja wa Kimataifa Songwe nje kidogo ya jiji la Mbeya baada ya kuzidiwa na ukungu mzito ulioambatana na mvua.

Ndege hiyo ilitarajiwa kutua leo saa 2.00 asubuhi, lakini  ilipofika anga la jiji la Mbeya ilikumbana na ukungu ulioambatana na mvua kubwa ikinyesha.

Kaimu meneja wa uwanja huo, Hamis Amiri  amesema marubani wa ndege hiyo waliamua kurudia Dar es Salaam na abiria ili kuepuka kufanya majaribio ya kutua jambo ambalo ni hatari.

‘Kwanza kulikuwa na mvua kubwa, halafu ukungu pamoja na mawingu yalitanda eneo la uwanja  jambo ambalo lilisababisha marubani washindwe kuona vizuri njia ya ndege licha ya kuwapo taa,’’ amesema Amiri.