Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

China yazidi kupunguzia kampuni kutoka nje masharti ya kuwekeza

Muktasari:

  • Muswada wa sheria inayoondoa urefu wa mchakato wa kuwekeza na masharti mengine yaliyokuwa yakilalamikiwa na kampuni za nje utajadiliwa na kupitishwa na Bunge la Watu wa China linaloanza kikao kesho.

Bunge la China litapiga kura wiki ijayo kupitisha muswada unaosubiriwa kwa hamu ambao una mabadiliko makubwa kwa wawekezaji wageni, ofisa mmoja amesema leo, hatua ambayo inaweza kusaidia kurahisisha biashara na Marekani.
Muswada huo wa sheria ya uwekezaji kutoka nje, utakuwa ni kitu kinachofuatiliwa katika kikao cha kila mwaka cha Bunge la China ambacho kitafanyika kwa wiki mbili kuanzia kesho.
Sheria hiyo inalenga kushughulikia malalamiko ya muda mrefu za kampuni za nje, ingawa mataifa ya Ulaya yanadai kuwa muswada huo unaharakishwa kukidhi mahitaji ya Marekani katika biashara.
Muswada huo ukipitishwa, utaondoa masharti yanayotaka kampuni za nje kuhamishia China umiliki wa kiteknolojia wa siri za ushindani wa kibiashara wakati zinapotaka kuingia katika ubia na kampuni za China, jambo ambalo limekuwa mjadala mkubwa katika mazungumzo na Marekani.
Pia inaahidi kuondoa urefu wa mchakato kwa kampuni za kigeni kuingia soko la China, msemaji wa NPC, Zhang Yesui alisema katika mkutano na waandishi wa habari.
Mabadiliko hayo yatahakikisha kuwa wawekezaji kutoka nje watapata upendeleo sawa na kampuni za China katika sekta zote, isipokuwa zile nyeti zilizoanishwa katika "orodha hasi".
China hutumia "orodha hasi" kuanisha maeneo ambayo hayatakiwi kuguswa na kampuni ambazo si za serikali au ambayo yanahitaji kampuni hizo kupitisha mchakato wa maombi na kusubiri yapitishwe.
"Maeneo ya kuzuia na kudhibiti kampuni za uwekezaji kutoka nje yataelezwa bayana na orodha hasi itakuwa wazi," alisema Zhang.
"Kampuni za China na za nje zitahudumiwa bila ubaguzi."
Sheria hiyo ambayo imeunganishwa itachukua nafasi ya sheria tatu kuhusu uwekezaji ubia kati ya kampuni za China na za nje.
"Hii ni hatua muhimu kwetu katika mfumo wa kusimamia uwekezaji kutoka nje, ambao utaongeza uwazi na ubashiri wa mazingira ya uwekezaji," alisema Zhang.