Uwanja wa ndege Saudi Arabia washambuliwa

Monday June 24 2019

 

Saudi Arabia. Waasi wa Houthi wa nchini Yemen wameushambulia uwanja wa ndege wa Abha ulioko Kusini Magharibi mwa Saudi Arabia.

Shambulio hilo lilotokea leo Jumatatu, June 24, limesababisha kifo cha mtu mmoja huku wengine saba wakijeruhiwa.

Taarifa ya Shirika la habari la serikali la Saudi Arabia (SPA), ilisema waasi hao wa Houthi walisema kwamba wamefanya mashambilizi ya ndege zisizotumia rubani katika viwanja vya ndege vya Abha na Jizan ambavyo vyote viko karibu na mpaka wa Yemen.

Hata hivyo, mpaka sasa Serikali ya Saudi Arabia haijatoa tarifa rasmi kuhusiana na shambulio hili wakati Muungano wa kijeshi unaongozwa na Saudi Arabia umeelezea tukio hilo kuwa ni la kigaidi.

Hii ni mara ya pili kwa kundi hilo kufanya mashambulizi ambako mapema mweiz huu waasi hao walipiga makombora katika uwanja wa ndege wa Abha na kujeruhi watu 26.

Advertisement