Watu 270 wafa wakisimamia uchaguzi Indonesia

Muktasari:

  • Ni baada ya kufanya kazi mfululizo bila kupumzika kwenye usimamizi wa uchaguzi Indonesia huku wengine 1878 wakiwa mahututi

Indonesia. Takriban wasimamizi 272 wa uchaguzi nchini Indonesia wamefariki dunia baada ya kuugua maradhi yaliyosababishwa na kufanya kazi zinazohusiana na uchaguzi kwa muda mrefu bila kupumzika.

Msemaji wa Tume ya Uchaguzi ya Indonesia (KPU), Arief Priyo Susanto amesema idadi hiyo ni hadi jana usiku huku wengine 1,878 wakiwa wanaugua maradhi hayo.

Susanto amesema Wizara ya Fedha hivi sasa inashughulikia kuzilipa fidia familia zao, watu hao waliopoteza maisha kwa maradhi yaliyochangiwa na uchovu huku ikiahidi kuwapa siku za mapumziko watumishi hao.

Uchaguzi wa Indonesia uliofanyika Aprili 17, 2019 ulihusisha kura ya rais, bunge na uchaguzi za serikali za mitaa. Wapiga kura takriban milioni 193 walishiki.

Uchaguzi huo unaotajwa kuwa mgumu ulihusisha wasimamizi takriban milioni sita katika vituo 810,000.