Wanamuziki wa kike, marapa watarajia makubwa tuzo za Grammy Jumapili

Saturday February 9 2019

 

Nyota wakubwa wa muziki duniani wanakutana Los Angeles kesho kwenye tamasha la kutuza wanamuziki la Grammy, na wafuatiliaji mwaka huu wanategemea wasanii wa hip-hop na wanawake watatamba.

Tamasha hilo la kila mwaka limekuwa likikosolewa na wadau ambao wanadai kuwa washindi wengi ni wasanii wenye ngozi nyeupe na wanaume, lakini kwa mwaka wa pili mfululizo wasanii weusi wa miondoko ya hip-hop walitawala orodha ya wanamuziki waliotajwa kuwania tuzo hizo kubwa duniani.

Rapa Kendrick Lamar -- ambaye alishinda tuzo ya Pulitzer Prize kutokana na albamu yake ya "DAMN" lakiniu hakuweza kushinda tuzo ya Grammy ya Albamu Bora ya Mwaka -- ametajwa kuwania tuzo nane, wakati rapa wa Canada, Drake anawania saba.

Wasanii wa kike pia wametajwa katika tuzo zote kubwa baada ya kuibuka patupu mwaka mmoja uliopita. Rapa Cardi B, nyota wa pop Lady Gaga, Janelle Monae na nyota wa muziki wa rock,Brandi Carlile ni miongoni mwa wanaoongoza katika tuzo hizo.

Katika kipengele cha Msanii Bora Mpya, wanamuziki sita kati ya nane waliotajwa, ni wanawake.

Lakini matarajio hayo yatakuwa sahihi kama wasanii hao watashinda tuzo hizo baada ya rapa tajiri, Jay-Z left kuondoka mikono mitupu mwaka jana licha ya kutajwa kuwania tuzo nane.

Jambo hilo liliibua mjadala mkubwa -- hata ushindi usiotarajiwa wa nyota wa miondoko ya funk, Bruno Mars ulionekana kugawanya watu, kwa kuwa ulionekana haukustahili mbele ya kazi nyingine zilizotamba.

Katika kukabiliana na hali hiyo, waandaaji wa tuzo za Grammy, Recording Academy waliunda kikosi kazi chenye watu wa aina tofauti na kuongeza tuzo kubwa kutoka nne hadi tano.

"Tasnia na taasisi ya Recording Academy wanaelewa kuwa wana tatizo mikononi mwao," Murray Forman, ambaye alisomea muziki wa pop katika Chuo kikuu cha Northeastern cha Boston, aliiambia AFP.

Wakati tamasha hilo likikaribia, ulikuwa ukizidi huku wasanii nyota kadhaa wakikataa kutumbuiza katika hafla hiyo itakayofanyika ukumbi wa Staples Centre.

Drake, Lamar na Childish Gambino wamesharipotiwa kukataa maombi ya kutumbuiza, wakati Ariana Grande amejiondoa kwenye shoo hiyo kutokana na kutofautiana na waandaaji katika masuala yanayohusu ubunifu.

Mata mtayarishaji wa tamasha la Grammys, Ken Ehrlich amekiri kuwepo kwa "tatizo" kuhusu nyota wa hip-hop ambao wanaona hawathaminiwi na Academy, ambayo inajumuisha watu 13,000 ambao ni wataalamu katika tasnia hiyo.

Kwa mara nyingine, Lamar ana nafasi ya kushinda tuzo kubwa ya Albamu Bora ya Mwaka baada ya kuikosa mara tatu -- safari hii kwa kutengeneza nyimbo katika filamu maarufu ya "Black Panther."

Wimbo wa filamu hiyo unaoongoza -- "All the Stars", ambao ameuimba pamoja na nyota wa miondoko ya R&B, SZA -- umetajwa katika tuzo ya Rekodi ya Mwaka, ambayo huenda kwa tuzo ya jumla ya wimbo bora, na Wimbo wa Mwaka, ambayo hutuzwa kutokana na uandishi.

Drake, ambaye awali alikuwa na tofauti na Recording Academy, ametajwa katika tuzo zote kubwa kutokana na albamu yake ya "Scorpion" na kibao kilichotamba mwaka jana cha "God's Plan."

Wanawake ni wa tano kati ya nane wanaowania tuzo ya Albamu ya Mwaka; Cardi B, Carlile, Monae, R&B prodigy H.E.R. na nyota wa muziki wa country, Kacey Musgraves.

Lady Gaga anawania tuzo tano, zikiwemo za Rekodi ya Mwaka na Wimbo wa Mwaka kutokana na wimbo wake wa "Shallow," ambao ametumbuiza kwenye filamu ya "A Star Is Born" akiwa na Bradley Cooper.


Advertisement