Beyonce aimba Kiswahili, wimbo wake kutumika kwenye filamu

Muktasari:

Mwanamuziki wa nchini Marekani, Beyonce Knowles ameachia wimbo mpya wenye mashairi ya lugha ya Kiswahili


Dar es Salaam. Mwanamuziki wa nchini Marekani, Beyonce Knowles ameachia wimbo mpya wenye mashairi ya lugha ya Kiswahili.

Wimbo huo ulioachiwa leo Jumatano Julai 10, 2019 unaitwa ‘Spirit’ na mwanamuziki huyo anasikika akimtaka, ‘uishi kwa muda mrefu mfalme’,  huku sauti nzito ikiitikia ‘uishi kwa’.

Wimbo huo umetumika katika filamu mpya ya Lion King inayotengenezwa na kampuni ya Disney ya nchini Marekani.

Mfalme anayeimbwa kwenye wimbo huo ni simba dume kijana anayeanza safari ya kupambana ili kuwa mfalme wa mbuga.

Disney wamesema albamu hiyo iitwayo ‘Spirit’ itatolewa siku tisa sijazo kuanzia leo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Disney ikimnukuu Beyonce imesema albamu hiyo imejumuisha vionjo vya waandaa muziki kutoka Afrika.

"Ni mchanganyiko wa kila kitu, si sauti moja tu. Kuna ushawishi kutoka kila kona, kutoka kwenye R&B, hip-hop na Afro Beat,”

 “Lengo langu halikuwa uimbwe na wasanii maarufu, bali utayarishwe na watayarishaji wa Afrika,” amesema Beyonce.