Gharama za matibabu ya Ruge zafikia Sh650 milioni

Muktasari:

Ruge Mutahaba kwa siku matibabu yake ni zaidi  Sh milioni tano hadi sita akiwa Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) lakini akiwa katika wodi ni Sh 1 milioni na hadi sasa gharama zilizotumika ni zaidi ya Sh650 milion na bado yupo hospitali.

Dar es Salaam. Gharama za matibabu ya Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds TV na Redio, Ruge Mutahaba zimeelezwa kufikia zaidi ya Sh650 milioni hadi sasa huku kila  siku akitumia kati ya Sh5 hadi Sh6 milioni.

Kwa muda sasa Ruge yupo nchini Afrika Kusini kwa matibabu ya figo na imeelezwa na mdogo wake, Mbaki Mutahaba kuwa kaka yake anaendelea vizuri.

Mbaki amesema mpaka sasa, Ruge ametumia kati ya Sh500 hadi Sh650 milioni kwa matibabu hayo na zaidi ya Sh530 milioni zimetolewa na Clouds Media.

Amesema gharama za matibabu ni kubwa lakini aliwashukuru watu mbalimbali wanaoendelea kujitolea kwa namna moja au nyingine.