Matibabu ya Ruge kwa siku Sh5 milioni, ndugu waomba msaada

Ruge Mutahaba 

Muktasari:

Ndugu wa Ruge Mutahaba wameomba msaada wa fedha kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu ya mkurugenzi huyo wa vipindi na uzalishaji waClouds Media Group.


Dar es Salaam.  Ndugu wa Ruge Mutahaba wameomba msaada wa fedha kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu ya mkurugenzi huyo wa vipindi na uzalishaji waClouds Media Group.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha Televisheni cha Clouds jana Jumatatu, Februari 18, Mbaki Mutahaba ambaye ni kaka wa mkurugenzi huyo alisema kwa sasa Ruge anapatiwa matibabu Afrika Kusini ambako kwa siku gharama ni Sh5milioni.

"Alianza kuumwa mwaka 2018, alilazwa katika Hospitali ya Kairuki  kisha akapelekwa India, sapoti ni kubwa tunashukuru na hata Rais (John Magufuli)  ametoa mchango na anaendelea, "alisema Mbaki Mutahaba

"Ana figo ambayo haipo sawasawa ilikuwa lazima wambadilishe. Madaktari wa hospitali ya Kairuki na Muhimbili wakashauri apelekwe Afrika Kusini maana ni karibu zaidi lakini gharama ni kubwa."

Ameongeza, "Kule (Afrika Kusini) mfumo wao wa malipo ni tofauti unapaswa kulipa fedha taslimu. Kuna namba rasmi imeandikishwa kwa jina la mdogo wetu Kemilembe Mutahaba unaweza kutusaidia."

Namba hiyo ni  0752 222210.