Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hukumu mvutano mazishi ya mawazo kesho

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, marehemu Alphonce Mawazo

Muktasari:

Baba mdogo wa Mawazo, Mchungaji Charles Rugiko alifungua kesi hiyo juzi kutokana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo kupiga marufuku shughuli za kuaga mwili wa marehemu aliyeuawa na watu wanaodaiwa ni wafuasi wa CCM Novemba 14.

Mwanza. Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kesho mchana inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi iliyofunguliwa na ndugu wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo wakipinga zuio la polisi kuchukua na kuaga mwili wa Mawazo kwa maelezo ya kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu.

Baba mdogo wa Mawazo, Mchungaji Charles Rugiko alifungua kesi hiyo juzi kutokana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo kupiga marufuku shughuli za kuaga mwili wa marehemu aliyeuawa na watu wanaodaiwa ni wafuasi wa CCM Novemba 14.

Usikilizaji wa kesi hiyo ulichukua saa tatu kutokana na uwapo wa mvutano wa kisheria  kwa mawakili wa pande mbili, ilianza kusikilizwa saa 5:00 asubuhi hadi saba adhuhuri na Jaji Lameck Mlacha.

Kesi hiyo namba 11 ya mwaka 2015, imevuta  hisia za watu wengi jijini Mwanza  mlalamikaji anaomba mahakama kuondoa zuio la Mkumbo kuzuia kuagwa mwili wa Mawazo; Kutoa tamko la zuio la Mkumbo kuwa ni batili na kinyume cha sheria na mahakama imkataze Kamanda Mkumbo kujihusisha na shughuli za mazishi na kuaga mwili huo.