Maswali 10 tukio la mkurugenzi mauaji kanisani

Muktasari:

Ni baada ya kudaiwa kuhusika katika mauaji ya mtu aliyekuwa akisali kanisani, hata hivyo kuachiwa kwake kumeibua maswali mbalimbali, mzazi aeleza mambo mazito

Dodoma. Unaweza kusema Jeshi la Polisi mkoani Singida ‘limemchomoa’ mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Pius Luhende katika tuhuma za kuhusika na mauaji ya Isaka Petro (28).

Taarifa ya polisi mkoani humo inaeleza kuwa watu saba wanashikiliwa akiwemo mkurugenzi huyo.

Haya ndio maswali 10 ya Mwananchi kuhusu tukio hilo;


1. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi alifuata nini kanisani?

2. Je, ni kweli mkurugenzi huyo ana ugomvi na baba wa marehemu?

3. Je, mkurugenzi ndiye aliyetoa bunduki na kumfyatulia Isaka Isaka na kumuua?

4. Polisi wanasema tukio la mauaji lilitokea wakati mkurugenzi akiwa amekimbia je, ni nani aliyefanya mauaji hayo?

4. Polisi wanasema mkurugenzi huyo alikimbia na kufunga mlango, kwa nini alifunga mlango wa kanisa?

5. Baba wa marehemu anasema alishuhudia mkurugenzi akifyatua risasi, nani anazungumza ukweli, baba au polisi?

6. Je, ni kweli kuna kesi mbili mahakamani kati ya mkurugenzi na baba wa mare-hemu?

7. Kulikuwa na ulazima wowote wa mkurugenzi na msafara wake kwenda kudai ushuru wa mashamba kanisani?

8. Je, ni kawaida kwa mkurugenzi kupita mtaani kudai ushuru kwa wananchi?

9. Ni kwa nini Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo ame-shiriki mazishi ya Isaka Isaka na kutoa ubani wa Sh1 milioni?

10. Je, ni kwa nini polisi, uongozi wa Singida haukutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari kuzungumzia sakata hilo lilipotokea siku hiyo?