VIDEO: Mvumbuzi wa Tanzanite afariki dunia

Muktasari:

Mtoto wa marehemu, Hassan Ngoma amesema baba yake Mzee Jumanne Ngoma amefariki leo Jumatano katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa anapatiwa matibabu 

Dar es Salaam. Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite, Jummane Ngoma amefariki dunia leo Jumatano Januari 30, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mtoto wa marehemu, Hassan Ngoma akizungumza na Mwananchi amesema, “Ni kweli Mzee amefariki leo jioni hii hapa Muhimbili,” amesema Ngoma

Hassan amesema kinachofanyika kwa sasa ni kuuhifadhi mwili wa baba yake kisha baadaye watatoa taarifa rasmi ikiwamo utaratibu wa msiba utakuwa wapi na mazishi yatafanyika wapi baada ya kikao cha familia.

Aprili 6 mwaka jana, Rais John Magufuli akizindua ukuta wa mgodi wa Tanzanite, Mirerani mkoani Manyara alimzawadia Sh100 milioni kama shukrani kwa mchango wake kwa kugundua madini hayo.

 

 

Endelea kufuatilia Mwananchi