Mwenyekiti NEC aapishwa kuwa wakili wa kujitegemea

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Mahakama ya Rufani, Semistocles Kaijage

Muktasari:

  • Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amewaapisha wahitimu 720 wa sheria ya mafunzo ya sheria kwa vitendo kuwa mawakili wapya  wa kujitegemea, akiwemo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) Jaji wa Mahakama ya Rufani, Semistocles Kaijage na majaji wengine wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu pamoja na wasajili wa mahakama hizo na mahakimu mbalimbali.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Mahakama ya Rufani, Semistocles Kaijage ameapishwa kuwa wakili wa kujitegemea.

Jaji Kaijage amesajiliwa kuwa wakili leo Ijumaa Julai 19, 2019 katika hafla ya kuwasajili mawakili wapya akiwa miongoni mwa mawakili wapya wa kujitegemea 720 waliokubaliwa na kusajiliwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma.

Katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sheria jijini Dar es Salaam, mbali na Jaji Kaijage wengine waliokubaliwa na kusajiliwa ni majaji wa mahakama ya rufani, mahakama kuu, wastaafu na walio kazini.

Katika sherehe hiyo ya kuwakubali na kuwasajili mawakili wapya tangu mwaka 1986, pia wapo wasajili wa mahakama ya rufani, wasajili wa mahakama kuu pamoja na mahakimu wa mahakama mbalimbali nchini.

Miongoni mwa majaji hao wa Mahakama ya Rufani ni; Kipenka Mussa, Stella Mugasha, Richard Mziray, Sivangilwa Mwangesi, Gerald Ndika, Jacobs Mwambegele na Ignas Kitusi.

Majaji wa Mahakama Kuu ni Sekela Moshi, Moses Mzuna, John Utamwa, John Mugetta, Patricia Fikirini, Mohamed Gwae, Mustapher Siayani Benedict Mwingwa na majaji wastaafu Aisha Nyerere na Salma Chikoyo.

Kwa upande wa wasajili, Amir Msumi, Zahra Maruma, Eddie Fussi , ambao ni wasajili wa Mahakama ya Rufani wakati wasajili wa Mahakama Kuu ni, Projestus Kahyoza, Charles Magesa, Frank Mahimbali, Victoria Nongwa na Sundi Fimbo.

Upande wa mahakimu ni Frank Moshi ambaye ni Hakimu mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Honorina Kambadu,