Nape azua gumzo mtandaoni kwa kuweka picha ya saa

Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye 

Muktasari:

Picha ya saa iliyowekwa na mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye katika ukurasa wake wa Twitter imezua mjadala mtandaoni


Dar es Salaam. Picha ya saa iliyowekwa na mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye katika ukurasa wake wa Twitter imezua mjadala mtandaoni.

Nape ambaye amewahi kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa CCM ameweka picha hiyo leo Jumanne Februari 5, 2019, ikiwa imepita siku moja tangu alipotangaza kujiuzulu  nafasi ya mwenyekiti  wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.

Kufuatia picha hiyo, watu mbalimbali wametoa maoni yao, wakiihusisha na masuala mbalimbali kutokana Waziri huyo wa zamani wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kutoeleza chochote katika ujumbe huo, zaidi ya kuweka saa hiyo pekee.

Jotham Leodgard’s ameandika  “Tunakumbushana tuu hiyo 12 unayoiiona hapo unatoa na hiyo 11 nyuma yake unapata jawabu la muda kiasi gani umebaki na vile vidoti pale mshale ulipokomea ndio miezi ya labda kutoka au kukumbukwa umuhimu wa wale waliomuweka, #TanzaniaYangu Mambo Mengi Muda mchache”.

Naye @Kirungi Amir‏  ameandika,” Nimekuamini upo kwa ajili ya Tanzania. Mwanaume usiyetanguliza tumbo lako. Nakuombea mafanikio”

Kwa upande wake @Jacobs King ameandika “Nyinyi mnamlisha Nnauye_Nape maneno, nafikiri anachomaanisha ni muda wa kumsikiliza Tundu Lissu Washington DC Marekani katika hutoba ya dunia.”

Naye @Muhidin Mkwera ameandika, “Kinachowaumiza ni kugeuza madhambi ya mtu kuwa ya chama, kwamba mnakubali kuumia na kuumiza wananchi kwa kulinda chama, weka saa weka alama ya chochote kile lakini tumbili ameshamaliza kula vya jirani sasa ameingia ndani mwenu. Ni kuchaguatu kumtoa kwa marungu au aendelee na shughuli.”

“Waswahili wanasema ni suala la muda tu,” ameandika @Mjeshi Msofe huku @Daudi S. Mkwela akiandika, “Nimekuelewa, una maanisha 2020 imekaribia.”