Ndege ya Dreamliner yatua nchini

Muktasari:

Ndege hiyo ni ya nne kuwasili kati ya saba zilizonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kuliwezesha Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL) kuimarisha huduma zake.

Dar es Salaam. Leo Jumapili Julai 8, 2018 saa 11:15 jioni ndege mpya ya Serikali aina ya Boeing 787-8 Dreamliner kwa mara ya kwanza imetua katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Ndege hiyo ni ya nne kuwasili kati ya saba zilizonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kuliwezesha Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL) kuimarisha huduma zake.

Rais John Magufuli, makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ni miongoni mwa viongozi  walioshiriki katika mapokezi ya ndege hiyo.