Necta yafuta matokeo kidato cha nne sekondari ya Tumaini Lutheran

Muktasari:

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limefuta matokeo ya wanafunzi 57 wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Tumaini Lutheran Seminari  ya Malinyi mkoani Morogoro baada ya kubaini shule hiyo kuvujisha mtihani huo


Dodoma. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limefuta matokeo ya wanafunzi 57 wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Tumaini Lutheran Seminari  ya Malinyi mkoani Morogoro baada ya kubaini shule hiyo kuvujisha mtihani huo.

Mbali na kufuta matokeo hayo, Necta imekifungia kituo hicho cha kufanyia mtihani.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Januari 24, 2019 na Katibu Mkuu mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde wakati akitangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 mkoani Dodoma.

Amesema wameagiza wahusika wote kuchukuliwa hatua wakiwemo polisi waliosimamia.

Dk Msonde ameanza kutangaza matokeo hayo leo saa 5:00 asubuhi.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.