RC Gambo aagiza kukamatwa maofisa halmashauri ya Meru

Mkuu wa mkoa Arusha Mrisho Gambo akiwa katika kikao cha mabaraza la madiwani wa Meru kujadilo ripoti ya CAG ambapo ameagiza kukamatwa maafisa waliopoteza vitatu vitatu vya risiti.
Picha Husna Issa

Muktasari:

  • Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini Tanzania kwa mwaka 2017/18, ilibaini vitabu vitatu vya makusanyo ya fedha vya Halmashauri ya Meru mkoani Arusha kutoonekana hali iliyomfanya Mkuu wa Mkoa huo, Mrisho Gambo kuagiza kukamatwa kwa waliosababisha upotevu huo.

Arumeru.  Mkuu wa Mkoa wa Arusha nchini Tanzania, Mrisho Gambo ameagiza kukamatwa maofisa wa idara ya fedha katika halmashauri ya Meru mkoani humo ambao walihusika na upotevu wa vitatu vitatu vya makusanyo ya fedha.

Akizungumza katika kikao maalum cha kupitia, ripoti ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) cha halmashauri hiyo jana Jumatano Julai 10, 2019, Gambo alisema watumishi waliosababisha vitabu hivyo vitatu kupotea wapelekwe polisi mara moja  ili kujulikana wahusika halisi wa upotevu wa vitabu hivyo.

"Kitendo hiki cha upotevu wa vitatu kinamaanisha ni wizi uliotendeka hivyo kufunga hoja hii ni wahusika kupelekwa mahakamani au vitabu hivyo viletwe  na hao pia waliotajwa wapo watu wengine nyuma,” alisema Gambo

Alisema jeshi la  polisi lifanye  uchanguzi wao utakaopelekea  kujua ukweli kuhusu upotevu huo na taarifa zitolewe ili kukomesha vitendo hivyo.

Awali, madiwani wa halmashauri hiyo wakichambua ripoti ya CAG, walisema imebaini upotevu wa vitabu vitatu vya mapato katika halmashauri ya Meru.

Akiwasilisha taarifa hiyo, mweka hazina wilaya wa halmashauri hiyo, Jolius Ndianabo  katika kikao maalimu cha Baraza la madiwani kupitia hoja ya mwaka wa fedha 2017/18 alisema suala hilo ni moja ya hoja za CAG.

Diwani wa Kikwe, Paul Shango alisema kitendo hicho cha upotevu wa kitabu kina jirudia kila panapofanyiwa uchanguzi na hivyo huu ni ugonjwa utakaoendelea ikiwa sheria haitachukuliwa.

"Wahusika wachukuliwe hatua ili kuondosha uteketeshaji wa mali za umma kwani vitabu hivyo ni uandikishwaji wa mapato ya umma," alisema

Mkurugenzi wa halmashauri ya Meru, Emanuel Mkongo alisema  wamejipanga kwa kuendelea kupata hati safi  na ambao wanataka kuwarudisha ny