VIDEO: Rais Kenyatta: Waliofanya shambulio la kigaidi wote wameuawa

Muktasari:

Shambulizi hilo lilianza kwa mlipuko uliofuatiwa na milio ya risasi katika hoteli ya Dusit katika eneo la Chiromo, mjini Nairobi


Nairobi. Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema magaidi wote waliofanya shambulio katika hoteli ya kifahari ya DusitD2 na kusababisha vifo vya watu 14, wameuawa.

Kenyatta ametoa kauli hiyo leo Jumatano Januari 16, 2019 wakati akihutubia Taifa kuhusu operesheni ya kupambana na magaidi waliovamia hoteli hiyo. Tukio hilo lililotokea jana Januari 15, 2019.

Amebainisha kuwa watu 700 wameokolewa na vyombo vya ulinzi na usalama, kwamba operesheni hiyo imekamilika na magaidi wote wameuawa.

Rais Kenyatta amesema watu  30  waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali mbalimbali za mjini Nairobi.