Rais Museveni, Kagame marafiki wanaozozana

Muktasari:

Rais Kagame alikiongoza kitengo cha ujasusi na kumsaidia Rais Museveni kuingia madarakani  1986


Mashirika. Rais Paul Kagame wa Rwanda na Yoweri Museveni wa Uganda wameishi pamoja kama ndugu huku wakisaidiana mambo kadhaa kuhusu kutafuta utawala wa nchi zao.

Rwanda imekuwa ikiishutumu Uganda kwa kuyasaidia makundi yanayopingana na Serikali yake, huku nayo Uganda imekuwa ikiwatuhumu baadhi nchini Rwanda kwa ujasusi. Tuhuma ambazo pande zote mbili zinakana kuhusika nazo.

Wachambuzi wanataja kwamba kauli hizi si nyepesi na pengine inaashiria kazi nzito iliyopo.

Ni marafiki wawili ambao wameishi pamoja kwa muda mrefu lakini sasa hivi wanaishi kama maadui kutokana na mgogoro unaoendelea baina yao kwamba .

Rais Kagame, alipata  mafunzo ya kijeshi katika mataifa tofuati ikiwemo nchini Uganda na Tanzania yaliyomfanya kuonekana kama mpanga njama mzuri wa kijeshi.

Ameishi kama mkimbizi katika nchi hiyo jirani Uganda kwa miaka mingi. Alikuwa mfuasi muasisi wa jeshi la waasi la Rais Yoweri Museveni mnamo 1979.

Alikiongoza kitengo cha ujasusi na kumsaidia Museveni kuingia madarakani mwaka 1986.

Lakini muungano wao uliingia dosari wakati wa vita vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya mwaka 1998 na 2003 wakati mataifa hayo mawili yalipounga mkono makundi hasimu ya waasi.