Shule za Zanzibar, Mara hoi matokeo kidato cha sita

Muktasari:

  • Shule ya Sekondari ya Nyamunga ya mkoani Mara imeshika namba moja kati ya shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018

Unguja. Shule ya Sekondari ya Nyamunga ya mkoani Mara imeshika namba moja kati ya shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018.

Matokeo hayo yametangazwa leo Alhamisi Julai 11, 2019 na katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde.

Katika orodha hiyo kuna shule nne za Mjini Magharibi  visiwani Zanzibar ambazo ni Kiembesamaki A Islamic, Mpendae, Tumekuja na Haile Selassie.

Nyingine ni Mondo ya mkoani Dodoma, Nsimbo ya Katavi, Eckernforde ya jijini Tanga na shule mbili za mkoani Mara za Bumangi na Buturi.