Wabunge waanza kupiga kura kupitisha bajeti ya Serikali 2019/2020

Muktasari:

Wabunge wa Bunge la Tanzania wameanza kupiga kura kupitisha bajeti ya Serikali ya mwaka 2019/2020 ya Sh33.1 trilioni

Dodoma. Wabunge 393 wa Bunge la Tanzania leo jioni Juni 25, 2019 wameanza kupiga kura kupitisha bajeti ya Serikali ya mwaka 2019/2020 ya Sh33.1 trilioni.

Bajeti hiyo iliwasilishwa Juni 13, 2019 na kuanza kujadiliwa Juni 17 hadi jana jioni.

Kuanzia leo saa sita mchana mawaziri walijibu hoja zilizoibuliwa na wabunge na kuhitimishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango na naibu wake, Dk Ashatu Kijaji.

Katika upigaji kura huo wa wazi wabunge hao wanapaswa kuikubali au kuikataa bajeti hiyo kwa kusema ndio au hapana.