Watalii 600,000 kutembelea Zanzibar

Wednesday May 15 2019

Waziri wa Habari, Utalii, Mambo ya Kale wa

Waziri wa Habari, Utalii, Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo 

By Haji Mtumwa, Mwananchi [email protected]

Unguja. Watalii 600,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani wanatarajiwa kutembelea Zanzibar mwaka huu.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Mei 15  na Waziri wa Habari, Utalii, Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi.

Amesema watalii hao watatoka katika mataifa mbalimbali duniani ikiwamo Ukraine.

Amesema watalii hao kwenda Zanzibar kunatokana na visiwa hivyo kuwa na amani na utulivu pamoja na vivutio vingi na kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kuhakikisha hali hiyo inadumishwa ili watalii zaidi waweze kuitembelea.

Advertisement