Wizi wa mifugo wawapeleka jela miaka 30

Monday April 15 2019

 

By Anthony Mayunga, Mwananchi [email protected]

Serengeti. Washitakiwa wanne kila mmoja amefungwa miaka 30 jela kwa wizi wa kutumia nguvu.

Waliokumbwa na adhabu hiyo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Serengeti mkoani Mara ni Mkami Chacha (35) Mwita Maro (37) Msumba Achere (33) Kihesa Kihesa (35) wakazi wa kijiji cha Borenga wilayani hapa.

Kabla ya hakimu Ismael Ngaile kutoa hukumu, waendesha mashitaka wa Jamhuri, Paskael Nkenyenge na Renatus Zakeo leo Jumatatu Aprili 15, kuwa kwa pamoja walipora ng'ombe 55 zenye thamani ya Sh16.5 milioni mali ya wakazi wawili wa Murito wilaya ya Tarime.

Hakimu Ngaile akitoa hukumu amesema kila mshitakiwa atakwenda jela miaka 30 na wote watalazimika kulipa Sh16.5 milioni.

Amesema milango ya dhamana iko wazi.

Advertisement