Mahakama yatengua amri kukamatwa Babu Tale

Babu Talle

Muktasari:

Katika hukumu iliyotolewa na Jaji Agustine Shangwa Februari 18, 2016 ndugu hao waliamriwa kumlipa fidia ya Sh250 milioni, mhadhiri wa dini ya Kiislamu

Dar es Salaam. Mahakama Kuu imetengua na kufuta amri ya kuwakamata na kuwafunga gerezani wakurugenzi wa Tip Top Connection Company Limited, Hamis Shaban Taletale maarufu Babu Tale na ndugu yake Idd.

Uamuzi wa kufuta amri hiyo ulitolewa juzi na Jaji Edson Mkasimongwa baada ya kujiridhisha kuwa haikuwa halali kutokana na mamlaka iliyoitoa kutokuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Februari 16 naibu msajili wa mahakama hiyo, Wilbard Mashauri aliamuru Babu Tale na nduguye Idd wakamatwe na kupelekwa kifungoni katika Gereza la Ukonga kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya mahakama na Aprili 4 alitoa na kusaini hati ya kuwakamata.

Soma Zaidi:

Katika hukumu iliyotolewa na Jaji Agustine Shangwa Februari 18, 2016 ndugu hao waliamriwa kumlipa fidia ya Sh250 milioni, mhadhiri wa dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kutokana na makosa ya kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.