Unyanyasaji wa kijinsia katika tasnia ya burudani

Muktasari:

  • Ingawa wengi hukutana na vikwazo hivyo wakati wakijaribu kutafuta njia ya kutoka, hata wasanii wakubwa wanapotaka kupewa nafasi kubwa hujikuta katika mtego huo.Mwananchi ilifanya mahojiano na baadhi ya wasanii na huu ndio ulikuwa mtazamo wao huku wakitoa sababu mbalimbali.

Tasnia ya burudani inaandamwa na jinamizi la unyanyasaji wa kingono. Harvey Weinstein, Bill Cosby, R Kelly ni baadhi ya wanaume wanaotuhumiwa kufanya vitendo hivyo.

Watu mbalimbali wameendelea kufunguka kuwapo kwa unyanyasaji wa kingono katika tasnia hiyo duniani na Mercy Johnson mwigizaji maarufu wa Nigeria amewahi kukiri kukutana na kadhia hiyo.

Ingawa wengi hukutana na vikwazo hivyo wakati wakijaribu kutafuta njia ya kutoka, hata wasanii wakubwa wanapotaka kupewa nafasi kubwa hujikuta katika mtego huo.Mwananchi ilifanya mahojiano na baadhi ya wasanii na huu ndio ulikuwa mtazamo wao huku wakitoa sababu mbalimbali.

Qeen Darleen

Anasema wasichana wengi wamekuwa wakijirahisisha kwa wanaume ili kupata wepesi wa kutoka kisanaa.

Anaeleza kuwa kuna athari kubwa ya kuwa mpenzi unayefanya naye kazi, kwani naye akikuona na mtu mwingine lazima ugomvi utokee na kusababisha asiwe huru.

Mwasiti

Kwa upande wake Mwasiti anasema kutongozwa katika Sanaa kupo, ila ni namna msichana utakavyojiweka ndivyo utajikuta unaingia katika mtego huo.

Alipouuzwa kama alishawahi kupata malalamiko hayo katika kipindi ambacho ni kiongozi pale Jumba la Kukuza Sanaa(THT), anasema hajawahi kufikiwa na jambo hilo na kuongeza kuwa huenda imechangiwa na kuwepo kwa uongozi madhubuti kwani msanii hupitia mikono mingi anapofika hapo na kutoka kwake si maamuzi ya mtu mmoja.

Maua Sama

Mkali wa kibao cha Iokote, Maua Sama anasema yeye hajawahi kupitia hilo, japokuwa anakiri amelisikia kwa wasanii wengine.

Kilichomuokoa zaidi kwake anasema huenda mtu aliyemuingiza kwenye Sanaa kuheshimika na watu wengi walio katika tasnia hiyo.

“Nadhani hilo limekuwa likiwapa woga watu naofanya nao kazi kuthubutu kunitongza wakihofia kumvunjia heshima.”

Rosa Ree

Msanii Rosary Robert maarufu kwa jina la ‘Rozaree’ anasema yeye ishamtokea sana, lakini mara nyingi huepukana na watu wa aina hii kwa kuacha kufanya nao kazi.

“Mimi nikishaona unaanza kuleta mambo ya mapenzi pamoja na kwamba nishakuelewesha kuwa sipo tayari, ninachofanya ni kusimamisha shughuli niliyokuwa nafanya na wewe au kutafuta jambo jingine la kufanya.”

Monalisa

Akiwa msanii mwenye tuzo takribani nne mpaka sasa katika tasnia ya filamu hapa bongo, Monalisa anasema mpaka hapo alipofikia ameshakutana na wanaume wakora wengi tu lakini anashukuru ameweza kukabiliana nao.

Monalisa ambaye jina lake halisi ni Ivyonne Cherry, anasema kikubwa unachotakiwa mwanamke ni kujiamini kwa jambo unalolifanya na kueleza kwamba ukizoea kutumia mwili wako kufanikisha malengo fulani wanaume watakuwa watu wa kukupiga danadana kwani ukweli ni kwamba huambiana.

Steve Nyerere

Ukiwa unadhani wanaotongozwa kwenye Sanaa ni wanaume tu utakuwa unajidanga, kwani hata kwa wanaume ipo hiyo.

Hapa Steven Mengere maarufu kwa jina la Steve Nyerere, anasema hata wao wanaume wanakumbana na hali hiyo ya kutakiwa kimapenzi tena wao tofauti ni kwamba wanaowataka ni wamama watu wazima wenye hela zao.

Hata hivyo anasema mtego huo kwake huuepuka kutokana na ukweli kwamba ni mtu mwenye uwezo wa kutafuta hela yake mwenyewe lakini anaeleza wengine huwa wakishindwa.

Hata hivyo Steve anabainisha watengeneza filamu na waongozaji ndio wanachangia hayo kwani kuna wanaokutana na wasichana katika maeneo ya burudani na kutembea nao kwa ahadi za kuwaingiza kwenye Sanaa, tabia ambazo anabainisha kuwa ndizo zimechangia kuua soko la filamu.

“ilifika mahali hawa waongoza filamu wakikutana na msichana mrembo kwenye kumbi za disco wanamuona anafaa kuuza cover la filamu yake, na ili wakati mwingine amapate anamuingia kwa lengo la kuwa na mahusiano naye.

“Mwisho wa siku ndio wanajikuta wanaookota vichaa, wehu na wadangaji waliokuja kuharibu sifa ya tasnia hiyo,”anasema Steve ambaye amekuwa akiiga sauti ay baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Abdu Kiba

Msanii wa Bongo Fleva Abdu Kiba anasema kazi ya Sanaa ina changamoto kubwa na kama usipokuwa makini unaweza kujikuta uanaooa na kuacha kila siku.

Katika kuepuka mitego hiyo anasema anapokuwa kazini anakumbuka kazi hiyo anaifanya kwa ajili ya familia yake kuwa na maisha mazuri, hivyo kama ni mashabiki kumshobokea yanabaki palepale juwaani.