Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbowe: Lissu amefanyiwa upasuaji mara 14

Muktasari:

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amefanywa upasuaji mara 14 na ataendelea kufanyiwa upasuaji mwingine ndani ya wiki mbili zijazo.

Babati. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amefanywa upasuaji mara 14 na ataendelea kufanyiwa upasuaji mwingine ndani ya wiki mbili zijazo.

Mbowe amesema hayo jana kwenye mazishi ya marehemu Philip Gekul, baba mzazi wa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul yaliyofanyika kata ya Dareda.

Alisema hali ya Lissu inaendelea kuimarika lakini aliumizwa sana kama walivyokuwa wanaeleza mara zote lakini na jambo la kumshukuru Mungu kwamba ameendelea kuimarika.

"Ameendelea kupata afya, akili zake ni timamu, madaktari kule wanafanya kazi kubwa kwelikweli kuendelea kumuudumia na ni matumaini yetu kuwa baada ya muda Mungu atamrejesha katika wajibu wake wa kulitumikia Taifa,"

Mbowe alizungumza hayo baada ya kueleza kuwa alitokea Nairobi kuangalia afya ya mbunge huyo ambaye alipigwa risasi Septemba 7 mwaka huu akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma.