Mbunge mwingine Chadema ahamia CCM

Aliyekuwa mbunge wa Monduli (Chadema), Julius Kalanga.

Muktasari:

Kalanga ametangaza uamuzi huo usiku, Julai 31, 2018 mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.


Dar es Salaam. Julius Kalanga amekuwa mbunge wa tatu wa Chadema kujiunga na CCM, baada ya Julai 28, 2018 mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara kutangaza kujiunga na chama hicho tawala.

Kalanga ametangaza uamuzi huo usiku, Julai 31, 2018 mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.

Katika maelezo yake mafupi, mbunge huyo wa Monduli amesema hataki kuwa kikwazo cha wananchi waliomchagua kupata maendeleo.

"Siwezi kuwa sehemu ya kukwamisha maendeleo ya wananchi wa Monduli. Ubunge si tatizo kwangu naweza kuwa mkulima au mfugaji ila si kuwa kikwazo," amesema Kalanga.

Mwingine aliyejiunga CCM kutoka chama hicho ni Dk Godwin Mollel (Siha). Baada ya Dk Mollel kujiunga na CCM alipitishwa kuwania tena nafasi hiyo na kuibuka na ushindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika Februari 17, 2018.

Soma Zaidi: