Ndanda Mtwara imewakazia Ndanda Dar

Saturday August 5 2017

 

By Thomas Ng'itu

Klabu ya Ndanda Mtwara imeiwekea ngumu Ndanda Dar es Salaam kwenda mkoani Mtwara kwaajili ya kuungana na kuwa timu moja.

Taarifa kutoka ndani ya Ndanda Dar zinadai kuwa timu hiyo imefika mkoani Mtwara takribani siku tatu, lakini hawajakutana na Ndanda Mtwara kwa lengo la kumaliza tofauti ya pande zote hizo mbili juu ya hatma ya vikosi hivyo.

MCL Digital iilipomtafuta afisa habari wa timu hiyo Idrissa Bandari kutaka kufahamu ukweli uliopo katika timu hiyo alisema Ndanda ipo moja tu na hakuna Ndanda nyingine na kisha kukata simu yake.

“Kaka Ndanda ipo moja tu inabidi ieleweke hivyo, hakuna Ndanda nyingine na kama ipo basi hiyo haifahamiki na haijulikani kwetu, lakini kamati yetu ya usajili inakaa leo (jana) hivyo kama kutakuwa na lolote basi tutawajulisha,” alisema.

Hata hivyo, ilifahamika kuwa timu hizo mbili zingefikia makubaliano kati yao baada ya Ndanda ya Dar kwenda kujiunga na wenzao wa Mtwara, lakini mambo yamekuwa tofauti na ilivyokuwa inatarajiwa.

Advertisement