Nyalandu amjulia hali Tundu Lissu Nairobi

Muktasari:

  • Amefika nchini Kenya kwa lengo la kumuona  Lissu

Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu akiwa na wabunge wa Chadema,  Peter Msingwa (Iringa Mjini), Godbless Lema (Arusha Mjini) na kulia ni mbunge wa zamani wa Nyamagana Ezekiah Wenje jiijini Nairobi nchini Kenya.

Nyalandu amekwenda Nairobi kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye amelezwa katika Hospitali ya Nairobi akiendelea na matibabu baada ya kujeruhiwa kwa risasi mjini Dodoma hivi karibuni.