Sabodo ataka kurejesha enzi za Mwalimu Nyerere

Sunday August 07 2016
pic sabodo

Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo.

Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo ameitaka Serikali kuwachangisha wananchi ili kupata fedha za kuhamishia makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.

Akizungumza jana katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam, Sabodo alisema hana fedha za kutoa kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa miundombinu mkoni Dodoma.

“Nataka niweke suala hili vizuri, sina fedha za aina hiyo popote pale. Ninazo mali kadhaa lakini sina fedha zote hizo. Watu wengi wanakuja kwangu, wanakuja hapa, nipe pesa, nipe pesa, hakuna pesa hapa,” alisema Sabodo na kuongeza:

“Mimi ni kama kichocheo tu, kama ndimu unatia kwenye soda. Nilichosema ni kutafuta juhudi kutoka kwa kampuni za India na Singapore kufanikisha ujenzi wa makao makuu ya Dodoma, lakini sina kiasi chote hicho cha fedha,” alisema.

Advertisement