Taasisi za fedha zinavyoigeukia sekta binafsi

Muktasari:

ziada kufanikisha mipango yao. Kwa muda mfupi, mambo mengi yame- jiri kwenye sekta hii ambayo yameanza kuonyesha matunda hata kwa wananchi wa kipato cha chini.

Kutoka kupunguza mikopo ya sekta binafsi kutokana na kupungukiwa ukwasi kwa miaka miwili iliyopita, taasisi za fedha na benki za biashara sasa zinashusha riba kwa wateja wake. Baada ya Serikali kuchukua hatua za kubana matumizi na kuongeza udhibiti kwa watendaji na watumishi wake, benki nyingi nchini zilipungukiwa ukwasi wa

ziada kufanikisha mipango yao. Kwa muda mfupi, mambo mengi yame- jiri kwenye sekta hii ambayo yameanza kuonyesha matunda hata kwa wananchi wa kipato cha chini.  Mapema mwaka jana, BoT ilishusha kiwango cha akiba ambacho benki za biashara zinatunza kwake kutoka asilimia 10 mpaka nane ili kuzipa uwezo zaidi wa kuikopesha sekta binafsi. Mwezi huu Benki ya CRDB imetangaza kushusha riba kwa asilimia nne kutoka asilimia 21 mpaka 17 huku ikiongeza muda

wa marejesho kwa mwaka mmoja ambao hata hivyo unatofautiana kati ya wafan- yakazi wa sekta binafsi na watumishi wa umma. Mabadiliko hayo yanalenga kumpa mte- ja unafuu wa kukamilisha malengo yake kwa wakati kwa kuwaruhusu watumishi wa umma ambao awali walikuwa wana- fanya marejesho mpaka miaka sita au miezi 72, sasa wafanye hivyo mpaka miezi 84 au miaka saba wakati wafanyakazi wa sekta binafsi waliokuwa na miaka mitano

wakiongezewa mpaka miaka sita. Mbali na CRDB, hivi karibuni, Bank of Africa (BoA) imetangaza kupunguza riba mpaka asilimia 11 kwa watumishi wa Seri- kali kwa mikopo ya kuanzia Sh1 milioni hadi Sh30 milioni.  Hatua hiyo ambayo inatajwa kuwa neema kwa watumishi wa umma ilitangazwa jijini Dodoma ambapo mkopaji atatakiwa kufanya marejesho ndani ya mwaka mmoja hadi mitano.

Kuunganisha benki

Alipokuwa akizindua tawi la Benki ya CRDB mjini Chato, Rais John Magufuli alisema Serikali haitatoa fedha kwa benki itakayosuasua, hivyo kuzitaka kuwa na mikakati endelevu.

Kutokana na msimamo huo wa Serikali, wiki iliyopita BoT ilitangaza kuziunganisha Benki ya Posta (TPB) na Twiga Bancorp. Uamuzi huo umefanywa baada ya Twiga kushindwa kujiendesha.

Naibu Gavana wa BoT, Dk Bernard Kibesse alitangaza uamuzi huo na kusisitiza: “Kuna haja ya kuwa na benki chache za Serikali ili kupata ufanisi wa huduma, huo ndiyo mwelekeo. Serikali haitasita kuziunganisha benki zake, hatua kama hii tuitarajie.”

Benki zafutwa

Kuunganishwa kwa TPB na Twiga kumefanywa baada ya kushuhudia benki tano zikifutiwa leseni baada ya kushindwa kujiendesha kutokana na kupungukiwa mtaji unaohitajika kisheria.

Mapema Januari, aliyekuwa Gavana wa BoT, Profesa Beno Ndulu alitangaza kuzifungia benki tano baada ya kujiridhisha kuwa hazina mtaji wa kutosha kujiendesha kwa mujibu wa sheria za usajili wa taasisi za fedha.

Taasisi zilizoathirika ni Benki ya Wananchi Njombe na Meru, Benki ya Ushirika Kagera, Benki ya Covenant na Ephata.

Profesa Ndulu alisema uamuzi huo unalenga kulinda masilahi ya wateja wenye amana katika taasisi hizo kwani kuziruhusu kuendelea kutoa huduma kunaweza kukasababisha kupotea kwa fedha za wateja hivyo kuwayumbisha kiuchumi.

Wakati benki hizo zikifutiwa leseni, nyingine tatu zilipewa muda kuhakikisha zinakidhi matakwa ya kisheria. Hizo zilikuwa ni Benki ya Chama cha Ushirika Kilimanjaro, Benki ya Wanawake (TWB) na Benki ya Wananchi Tandahimba.

Kati ya benki nne zilizokuwa chini ya uangalizi wa BoT, ni Twiga pekee imepata namna ya kuondoka kwenye hali hiyo na kuziacha tatu zikiendelea kujipanga.

Fedha za Serikali

Kuyumba kwa mtaji wa baadhi ya benki kunatokana na mambo mengi yaliyojiri tangu mwishoni mwa mwaka 2015. Mapema mwaka 2016, Serikali ilitangaza kuhamisha akaunti za mashirika na taasisi zake kutoka benki za biashara kwenda Benki Kuu (BoT).

Kutokana na uamuzi huo, benki hizo zilipoteza zaidi ya Sh700 bilioni zilizokuwa zinatunza kutoka taasisi mbalimbali za umma.

Profesa Ndulu alisema uamuzi huo umesaidia kupunguza riba za mikopo kutoka wastani wa asilimia 15.49 hadi asilimia 13.87.

Kutokana na uamuzi huo, benki nyingi zilizokuwa zinatunza fedha hizo ziliathirika kiasi cha kupunguza mikopo inazotoa hasa kwa sekta binafsi.

Riba ya BoT

Mwaka jana, BoT ilishusha riba za mikopo inayotoa kwa taasisi za fedha na benki za biashara nchini. Vilevile, imepunguza kiasi cha fedha ambazo taasisi hizo zinapaswa kutunza BoT kwa mujibu wa sheria.

Machi mwaka 2017, ilipunguza riba hiyo kutoka asilimia 16 hadi 12 na Agosti ikashusha tena hadi asilimia tisa ili kuzishawishi benki hizo kuongeza mikopo zinazotoa kwa sekta binafsi.

Mabadiliko hayo, pamoja na mambo mengine yalikusudia kuhakikisha benki za biashara zinakuwa na fedha za kutosha kujiendesha.

Kuhamisha fedha za Serikali, kupunguzwa kwa wafanyakazi wasio na vyeti pamoja na watumishi hewa na kufungwa kwa baadhi ya biashara ni miongoni mwa mambo yaliyoiathiri sekta ya fedha mwaka huo.

Mikopo chechefu

Ndani ya miaka miwili iliyopita, sekta ya fedha nchini ilikabiliwa na ongezeko la mikopo chechefu (NPL) ambayo pamoja na sababu nyingine ilichangiwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali kudhibiti matumizi yake.

Uamuzi wa Serikali kuwafuta kazi watumishi wake takriban 10,000 walioghushi vyeti kuliongeza idadi ya mikopo isiyolipika.

Baadhi ya watumishi hao walikopa kwenye taasisi za fedha kwa dhamana ya mishahara yao.

Mpaka Desemba 2016, uwiano wa mikopo chechefu kwa jumla ya mikopo yote ulikuwa wastani wa asilimia 9.5 ukiwa umepanda kutoka asilimia 6.4 kipindi kama hicho mwaka 2015, juu ya kinachopendekezwa na kanuni za Benki Kuu za mwaka 2006 ambacho ni asilimia tano.

Katika mikakati ya kushusha mikopo isiyolipika, taasisi hizo zilipunguza mikopo kwa sekta binafsi. Kupungua kwa mikopo hiyo ambayo mwaka 2015 iliongezeka kwa asilimia 26.8 mpaka asilimia 2.5 mwaka jana kulipunguza faida.

Wadau

Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti wa Taasisi ya Repoa, Dk Abel Kinyondo anasema uamuzi wa Serikali kuhamisha fedha zake kutoka benki za biashara ulikuwa mzuri ingawa benki ziliumizwa kwa kuwa ulifanyika haraka.

Anasema uzuri unatokana na Serikali kutawala sekta ya fedha nchini na kila benki ilitamani kufanya nayo biashara, jambo ambalo liliinyima fursa sekta binafsi ambayo ndiyo muhimu kwa maendeleo ya watu na Taifa.

“Benki zilikuwa hazijajipanga ndio maana zililalamika, lakini nchi nyingi zimewahi kufanya hivyo ikiwemo Rwanda na mambo yakaenda vizuri tu. Lengo la Serikali ni kutoa fursa kwa wajasiriamali kukopa ili kuendeleza uchumi wa nchi,” anasema Dk Kinyondo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye anasema mpango wa Serikali kuunganisha benki zake ni mzuri ambao hata benki binafsi zinapaswa kufanya, hivyo endapo wamiliki wataridhiana kwani kutaimarisha sekta hiyo nchini.

Simbeye anasem suala la benki za biashara kupunguza riba za mikopo halina tija kubwa kiuchumi kwani zimepunguzwa kwa watumishi na si wawekezaji wala wajasiriamali ambao ndiyo wanaojenga uchumi.

“Nasikia benki kadhaa zimepunguza riba ya mikopo lakini ukweli ni kwamba sio kwa sekta binafsi. Labda ahueni yetu ni kupungua kwa amana za Serikali (treasure bills) labda benki sasa zitaelekeza mikopo kwa sekta binafsi,” anasema Simbeye.