Wanawake ‘waliotelekezwa’ wapewa namba, watakiwa kurejea tena Ijumaa
Muktasari:
Wanawake hao walianza kusikilizwa jana
Dar es Salaam. Unaweza kusema idadi ya wanawake wenye watoto ‘waliotelekezwa’ waliofika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda leo Aprili 10, 2018 imezidi kuwa kubwa, sasa wameanza kupewa namba na kutakiwa kurejea tena ofisini hapo Ijumaa.
Mmoja wa maofisa wanaowasikiliza akinamama hao ameonekana akiwapa namba na kuwataka kurejea tena Ijumaa kwa ajili ya kusikilizwa.
Wanawake hao walianza kusikilizwa jana na kutokana na wingi wao uchukuaji wa malalamiko utafanyika kwa siku tano na ikishindikana zitaongezwa na utawekewa utaratibu ili watu wote wapate huduma.