Wanawake kuongeza nguvu Chadema

Wajume wa kikao cha Kamati ya Utendaji cha Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) wakiimba wakati wa ufunguzi wa kikao hicho kilichoanza jijjni Dar es Salaam, jana. Picha na Anthony Siame

Muktasari:

  • Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema  jana alipofungua mkutano wa Kamati ya Utendaji ya Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha).
  • Dk Mashinji amesema uongozi wa Serikali ya sasa, awali ulijinadi kwa kupambana na rushwa lakini kutoka na ugumu wa maisha uliojitokeza kiwango cha vitendo vya hivyo kinaweza kuongezeka.

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejipanga kuwatumia wanawake wenye uwezo kisiasa ili kuing’oa CCM madarakani mwaka 2020.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema  jana alipofungua mkutano wa Kamati ya Utendaji ya Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha).

Dk Mashinji amesema uongozi wa Serikali ya sasa, awali ulijinadi kwa kupambana na rushwa lakini kutoka na ugumu wa maisha uliojitokeza kiwango cha vitendo vya hivyo kinaweza kuongezeka.

Awali, Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Halima Mdee alisema chama hicho kinapaswa kujipanga vyema wakati wa uchaguzi kwa kuwatunza kwa macho sawa wagombea wanawake na wanaume ili kujihakikishia ushindi.

“Kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, wanawake tisa ndiyo waliopata ridhaa ya kugombea kwenye majimbo, kati ya hao sita walifanikiwa kushinda wakiwamo wawili walioshinda kwenye majimbo yanayotajwa kutawaliwa na mfumo dume. Unaweza kuona nguvu ya ushindi ilivyokuwa hata kwenye udiwani,” amesema Mdee.